DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya kesi ya jinai iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Luqman Maloto, kuhoji ukimya wa mamlaka za Serikali dhidi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, akidai kwamba Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, haina mamlaka ya kuisikiliza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pingamizi hilo limewekwa mahakamani hapo leo tarehe 8 Februari 2023 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, wakati kesi hiyo Na.5/2023 ilipoletwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Jaji John Nkwabi.

Baada ya Wakili Nkwabi kuwasilisha taarifa ya kusudio la kuweka mapingamizi hayo, Jaji Nkwabi ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 22 Februari mwaka huu, ambapo yataanza kusikilizwa kabla ya kesi hiyo kutajwa.

Pingamizi hilo ya DPP yamebeba hoja sita, ikiwemo mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi hayo, hati ya kiapo cha maombi hayo kuwa na dosari za kisheria ziszioweza kutibika na maombi hayo kutokuwa na uwezo kisheria.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad