Ticker

6/recent/ticker-posts

Mshika Nyoka auawa na Nyoka

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAMshika nyoka na muuzaji wa dawa za asili  za kujikinga na nyoka mkoani Lindi, Bw Japokuwa Masawila amefariki dunia baada ya kugongwa na nyoka ambaye alidhamiria kumdhibiti 
Mshika nyoka huyo ambaye ni maarufu kama Japo Manyoka, alijeruhiwa na nyoka akiwa katika mapambano makali ya kumdhibiti licha ya kubanwa na nyoka mara kadhaa, awamu hii imekuwa ngumu kwake kunusurika

Ndugu wa karibu wa Marehemu wamesema Japokuwa aliaga kwenda wilayani Kilwa kwaajili ya maonyesho yake ya Nyoka ili aweze kuuza dawa za kinga, lakini kwakuwa ni kawaida yake kuweka kambi sehemu na kutafuta nyoka wasumbufu katika maeneo anayofikia, alifanikiwa kupambana na nyoka ambaye mpaka sasa hajajulikana na wa aina gani ambaye alimjeruhi na kumfanya aishiwe nguvu na kumsababishia kifo

Baada ya Marehemu kuona hali yake kiafya si nzuri, aliwapatia majirani katika eneo hilo Namba ya simu ya mtoto wake pamoja na ya mkewe (mtaliki) ili wajuzwe lakini hawakuwahi kufanya naye mazungumzo zaidi ya kuambiwa tayari ameshafariki.

Naye mwenyekiti wa mtaa katika eneo alilokuwa anaishi mshika nyoka huyo anasema, taarifa ya kufariki kwa Mkazi wake ameipata mapema asubuhi ya leo na kwakuwa Bwana Japo alikuwa na kawaida ya kukaa na Nyoka katika eneo lake la makazi, yeye na viongozi wengine wa serikali wamefanya upekuzi katika chumba alichokuwa anakitumia marehemu kuhifadhi wanyama hao na kwa bahati mazingira yameonekana ni salama.

Majirani, wanasema Japo ni mtu wa ajabu kwani hakuwa akifanana na tabia za wengine walioweza kucheza na nyoka. Alihifadhi wanyama hao kwa siri na mara nyingi alikuwa mcheshi kwa watu wote.

Marehemu anatarajia kuzikwa Nyumbani kwao Mkoani pwani huku Serikali kupitia ofisi ya Maliasili Mkoani Lindi ikisema, eneo la makazi yake ni salama na hakuna hatari yoyote, lakini mifugo yake haiwezi kurithiwa hivyo itachukuliwa kwaajili ya usalama na kuihifadhi kwani bado ni mali za Asili
 

Post a Comment

0 Comments