Risasi Zimempa Maisha Dereva Wangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kufa kufaana, ndivyo tunavyoweza kusema baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu kudai Dereva wake ambaye alikuwa naye siku ya tukio wakati akipigwa risasi Septemba 17, 2027, Adam Bakari kupata kazi na kuishi nchini Ubelgiji.

Lissu, ambaye alikuwa akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media hii leo Februari 4, 2022 amesema, mara baada ya kutokea kwa tukio hilo Adam hakujua afanye nini na Polisi walipoanza kumtafuta kwa nia ya kumhoji aliogopa kutokana na vyanzo mbalimbali kudai kuwa naye angepotea hivyo kuamua kusafiri hadi Nairobi nchini Kenya kuepuka majanga.


Aliyekuwa Dereva wa Tundu Lissu siku ya tukio, Adam Mohamed Bakari.
“Dereva wangu alikuwa hajawahi kutoka Tanzania, kabla ya mimi kushambuliwa hakuwa na paspoti wala chochote na yalipoanza kutoka toka maneno tukimpata Dereva wake hadithi ya Mbowe itakamilika, Dereva apatikane afanywe aongee na atarekodiwa video aseme ni Mbowe kwahiyo ikambidi aje Nairobi akakaa nami,” anasimulia Lissu.

Aidha amebainisha kuwa, “sasa ikafikia kipindi mimi natakiwa kupelekwa Ulaya kwa matibabu tukauarifu ubalozi wa Ubelgiji na akapatiwa viza ya kibinadamuda kwenda pahala pengine na utaratibu wake wa maisha ya Ubelgiji yalikuwa tofauti na ya kwangu wakamtunza kumfundisha lugha na kumpatia kazi yaani kitu kibaya kilichonitokea kimezaa matunda mema kwake.”


Mwandishi wa Dar24 Media, Stanslaus Lambat akiwa katika mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu.
Alipoulizwa na mwandishi kuhusu ukimbiaji wa mapambano kwa kwenda nje ya nchi na kama wana uwezo wa kuiomboa nchi kama anavyodai, Lissu alisema anayepigana na kukimbia anaishi ili aweze kupigana na kesho maneno ambayo ameyanukuu toka kwenye wimbo wa marehemu Bob Malrey wa “‘He who fights and run away, live to fight another day”.

Aidha lissu amesema, katika mazingira ya nchi yenye watu masikini, viongozi hawatakiwi kuishi kifalme kwa kutembea na misafara yenye msururu wa magari na kuishi maisha ya anasa kitu ambacho kinawanyonya wananchi na kutoa ushauri wa kupunguza gharama za kuendesha Serikali.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad