Freeman Mbowe Apongeza Jeshi La Polisi Kwa Kuendelea Kulinda Mikutano Yao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kulinda mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani, huku akiwaahidi Askari Polisi kwamba chama chake kikiingia madarakani kitaendelea kulinda maslahi yao.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chadema, uliofanyika tarehe 27 Februari 2023, mkoani Njombe, Mbowe amesema Jeshi la Polisi kwa sasa limebadilika kwa kuwa na utu dhidi ya vyama vya upinzani, tofauti na ilivyokuwa miaka saba iliyopita.


“Tunawaahidi Polisi siku chama chetu kitaongoza dola, hatutaagiza Polisi kutoka Congo au Kenya, ni ninyi ambao vijana wetu mtakaoendelea na wajibu wenu. Msiipendelee Chadema, wala chama chochote cha siasa. Simameni katika kweli na haki,” amesema Mbowe.


Amedai kuwa, mabadiliko hayo yanatokana na kiongozi aliyekuwa madarakani kukomesha vitendo vya kikatili.


“Ndani ya wiki moja tumezunguka kufanya mikutano ya hadhara, nikiangalia jeshi la polisi silielewi, najiuliza hivi jeshi hili lenye ubinadamu huu ndiyo lilelile lililokuwa miaka saba iliyopita? Au limebadilika, hii maana yake kiongozi wa taifa sio jambo la masihara, mkiwa na kiongozi mkatili anatengeneza mfumo mzima wa ukatiili,” amesema Mbowe na kuongeza:


“Kwa miaka saba iliyopita tuliwaona adui wa taifa letu, tumetembea kote hakuna wa kutusumbua. Wametusindikiza wameonyesha ushirikiano bila ubaguzi.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad