Hatimaye Jeshi la Polisi Wafunguka Kuhusu Mauaji ya Martha Mfanyakazi wa BOA Bank Aliyouawa Pwani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limesema linafanya uchunguzi wa tukio la Watu wasiojulikana kummwagia mafuta yanayodhaniwa kuwa ni Petroli na kisha kumchoma moto na kumsababishia kifo Mwanamke aitwaye Neema Towo au kwa jina jingine Martha (30) Mfanyakazi wa BOA BANK Tawi la Kahama, Shinyanga ambaye pia alikuwa Mkazi wa Kwa Mbonde, Kata ya Kwa Mathias, Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

RPC wa Pwani, Pius Lutumo amesema “Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Raia wema, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumchukua Mhanga na kumpeleka katika Hospitali ya Tumbi kwa matibabu na baadaye Mgonjwa huyo alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uangalizi zaidi wa kimatibabu na alifariki usiku wa kuamkia Alhamisi March 09,2023”

“Kutokana na tukio hili kuwapo kwa mazingira yenye utata juu ya kifo cha Mhanga huyu, Makachero wetu wameanza ufatiliaji ili kuweza kubaini sababu za kuchomwa moto Mwanamke huyo na kupelekea kifo chake”

Unaweza kufuatilia habari hii kwa urefu kwenye Youtube ya millardayo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad