Jeshi la Polisi Lafunguka Sakata la Askari Anayedaiwa Kuwa Shoga Baada ya Video Kusambaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Polisi Shoga

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad amesema kuwa jeshi hilo linamchunguza askari wake ambaye anadaiwa kuonekana kwenye kipande cha video akifanya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).


Kamanda Hamad amesema kuwa endapo watabaini bila shaka kuwa askari huyo anajihusisha na vitendo hivyo, atafukuzwa kazi na kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama ya Kijeshi.


“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kadhia hiyo ikiwemo kumfanyia vipimo askari huyo ili kujiridhisha kama anafanya vitendo hivyo, ingawa tumeona video katika mitandao ya kijamii hatuwezi kusema moja kwa moja kuwa ni kweli au sio kweli,” Nipashe linamkariri Kamishna Hamad, leo.


Aliongeza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria, utamaduni na utaratibu wa jeshi la polisi hivyo hakiwezi kuvumilika. Akizungumzia madhara ya vitendo hivyo kwa askari, Kamishna Hamad alisema kuwa inapunguza heshima kwa jeshi la polisi na kuondoa ukakamavu kwa askari.


Aidha, alisema jeshi hilo linampango wa kufanya operesheni maalum ya kuwabaini askari wenye hulka hiyo ili kuwachukulia hatua stahiki.



Aliwataka wananchi kutohusisha vitendo hivyo na jeshi la polisi kama taasisi, kwani vinafanywa na askari ambao wengine huenda walianza vitendo hivyo wakiwa wadogo na baadaye wakajiunga na jeshi.


“Hata hizo picha hazioneshi kuwa amevaa sare za polisi, au ametenda kitendo hicho kwenye kituo cha polisi… kwahiyo, isitafsiriwe kuwa ni Jeshi la polisi ndio limefanya,” Kamishna Hamad anakaririwa.



Kiongozi huyo aliwataka askari wote kuzingatia sheria na kulinda heshima ya jeshi hilo, kwakuwa atakayebainika kufanya vitendo vyovyote kinyume cha maadili na kinyume cha sheria ikiwemo vitendo vya ushoga atafikishwa kwenye Mahakama za kijeshi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad