Kijana wa Miaka 17 Aiba Ndege ya Jirani yake na Kuipaisha Kisha Kuanguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kenya. David Chege kijana mdogo mwenye umri wa miaka 17, amewaacha watu vinywa wazi baada ya kuiba ndege ya jirani yake iliyokuwa imepaki na kuirusha bila woga, tovuti ya TUKO imeripoti.

Siku ya Ijumaa Machi 24, Chege anadaiwa kuingia kwa siri kwenye nyumba ya jirani yao ambaye ni mzungu na kufaulu kufika eneo la rubani na kufanikiwa kuiwasha kisha kuruka nayo kwa dakika kadhaa kabla ya kuparamia miti.

Mwenye ndege hiyo yenye usajili wa nambari 5Y-AZA aina ya PA25 aliwambia polisi kuwa kijana aliingia kwake asubuhi kinyemera na kutekeleza uharifu huo.

Iliripotiwa kuwa mwenye ndege hiyo ambaye ni mkaazi wa Balolow eneo la Ndume Gilgil alisema "saa 9:30 asubuhi kuna mtu aliingia kwake na kuipaisha ndege iliyokuwa imeegeshwa," taarifa ya polisi ilisema.

Katika taarifa nyingine mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi ameahidi kuhakiksiha kuwa atamsimamia Chege kusoma urubani.

"Naomba serikali kumsamehe huyu kijana kutoka Gilgil asishtakiwe, tafadhali mnipatie ili nimpeleke katika chuo cha kujifunza mambo ya kuwa rubani," alisema Sudi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad