Ticker

6/recent/ticker-posts

Mtoto wa Rais Museveni Atangaza nia ya Kumrithi Urais Baba yake

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba ametangaza nia ya kutaka kumrithi Baba yake kwenye kiti cha Urais wa Uganda ambapo amesema atagombea Urais wa Nchi hyo mwaka 2026.

"Katika jina la Yesu Kristo, kwa jina la Vijana wa Uganda na Dunia kwa ujumla na katika jina la Mapinduzi makubwa nitagombea Urais mwaka 2026"

"Fidel Castro Shujaa wangu alikuwa Rais akiwa na umri wa miaka 32, ninakaribia kufikia miaka 49, sio sawa kabisa (Kutokuwa Rais), Vijana wanapaswa kuwa Marais wa Mataifa yao"

"Nani anakubaliana na Mimi kwamba muda wetu Vijana umewadia?, inatosha sasa kuendelea kuongozwa na Wazee na kututawala, ni muda wa Vijana kung'aa, Waziri Mkuu wa Uingereza ana miaka 42, Waziri Mkuu wa Finland ana miaka 37, sisi wengine tunakaribia miaka 50, tumechoka kusubiri, nitasimama kugombea" amesema Muhoozi ambaye ni Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda.

Post a Comment

0 Comments