Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanafunzi Auawa Baada ya Kushinda Mchezo wa Bahati Nasibu

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA

 


Mwanafunzi wa shule ya sekondari Mchanganyiko nchini Kenya, Syengo Nyamai, aliyekuwa akisoma kidato cha pili mwili wake umepatikana akiwa ameuawa na kutelekezwa katika kichaka ikiwa zimepita wiki mbili tangu kijana huyo kushinda mchezo wa bahati nasibu pesa za Kenya shillings 200,000 ni zaidi ya milioni 3.5 za kitanzania.


Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17, alitoweka nyumbani kwa siku kadhaa mara baada ya kushinda bahati nasibu hiyo ya mchezo katika fainali ya kombe la #Carabao uliochezwa kati ya Manchester United dhidi ya Newcastle united.


Kaka wa marehemu amedai kuwa mdogo wake alitumia kitambulisho cha taifa cha jirani yao kusajili laini ambayo aliitumia katika kujiandikisha kwenye mchezo huo, hivyo basi polisi nchini humo wanaendelea kufanya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo.

Post a Comment

0 Comments