Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwijaku Amchana Diamond Platnumz "Badilisha Gari Au Rudi Kwa Zari Hassan"

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA

 

Mwijaku Amchana Diamond Platnumz "Badilisha Gari Au Rudi Kwa Zari Hassan"

Mhamasishaji katika mitandao ya kijamii hasa Instagram, @mwijaku amemtaka nyota wa muziki @diamondplatnumz kubadilisha aina ya gari anayoitumia na kama atashindwa basi arudi kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari The Boss Lady’


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwijaku ameandika

“Ili kukuwa zaidi nadhani huu ni wakati sahihi wa Mwambino (Diamond) kubadili gari, hata ukifuatilia ulimwenguni watu wanaokua kibiashara hawatumii gari zaidi ya miaka miwili” Mwijaku


Mwijaku ameendelea kukazia suala hilo akimtaka nyota huyo kubadili gari na sio wanawake na kama ikishindikana arudi kwa Zari.

“Haiwezekani mimi muajiriwa wako nabadili gari, wewe unabadili wanawake tu bila faida, au urudi tu kwa Zari” Mwijaku

Post a Comment

0 Comments