Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Samia ajibu utani wa Simba na Yanga fursa ya goli moja Milioni 5

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo akiwa Dar es salaam katika Sherehe za maadhimisho ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), amesema bado zile milioni tanotano za kununua magoli ya Simba na Yanga kwenye mechi za kimataifa zipo.

“Niwapongeze Wanangu wa Yanga na Simba kwa kuitumia vizuri fursa niliyowapa ya goli moja milioni 5 wameitumia vizuri sana, kwa hesabu nilizonazo nadhani Yanga wameshalamba milioni 30 na Simba jana milioni 35 na nyuma nadhani walikula 5 kwahiyo niwapongeze kwa kuitumia vema fursa hii, niwapongeze na ni imani yangu kwamba ile kasi iliyopo miguuni ya milionk 5 kwa goli itaendelea kuwepo huko mbele milioni 5 zitakapoondoka”

“Kwa sasa hivi niwahakikishie wale waliokuwa wakitania jana, niliona utani nampigia Msigwa namwambia ‘ebu maliza mpira haraka mimi pesa zimeisha’, nataka niwahakikishie kwamba Mama bado anazo wekeni mipira kwenye wavu jengeni jina la Nchi yetu, bado zipo” — Rais Samia

 

Post a Comment

0 Comments