Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Samia amwondoa Kusaya Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Makatibu Tawala wa Mikoa watatu (3) na kuwahamisha vituo vya kazi wengine watatu (3).


Rais Samia pia amemteua Ally Senga Gugu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, kabala ya uteuzi huu, Gugu alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na amemteua Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Willy Machumu ambave amestaafu.


Rais pia amemhamisha Fatuma Ramadhani Manga, kutoka Mkoa wa Dodoma kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida akichukua nafasi ya Dorothy Aidan Mwaluko ambaye amestaafu, Rashid Kassim Mchata, amehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani akichukua nafasi ya Zuwena Omari Jiri ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi akichukua nafasi ya Ngussa Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Post a Comment

0 Comments