Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Samia ateua makatibu tawala wa mikoa, Kamishna DCEA

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPARais Samia ateua makatibu tawala wa mikoa, Kamishna DCEA
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa watatu akiwemo Gerald Kusaya ambaye awali alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA).

Pia, Rais Samia amewabadilisha vituo vya kazi makatibu tawala wa mikoa sambamba na kumteua Kamishna mpya wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo ambaye anachukua nafasi ya Kusaya.

Uteuzi huo ni mwendelezo wa mabadiliko ambayo Rais Samia amekuwa akiyafanya kwa kuteua watu wapya na kuwabadilisha wengine vituo vya kazi, lengo likiwa ni kuimarisha utendaji wa kazi wa Serikali kama alivyoahidi Desemba 8, 2022 wakati wa mkutano mkuu wa CCM, Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 16, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amemteua Kusaya kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa akichukua nafasi ya Rashid Mchata ambaye amehamishiwa mkoa wa Pwani.

Wengine walioteuliwa ni Ally Senga Gugu ambaye anakuwa Katibu Tawala wa mMkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Dk Fatuma Mganga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Singida ambako nafasi hiyo imebaki wazi baada ya aliyekuwa katibu tawala wa mkoa huo, Dorothy Mwaluko kustaafu.

Vilevile, amemteua Tixon Nzunda kuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Willy Machumu ambaye amestaafu.

Wengine waliohamishwa vituo vya kazi katika mabadiliko hayo ni pamoja na Mchata ambaye anakwenda mkoa wa Pwani. Mchata pia aliteuliwa na Rais Samia kuwa Skauti Mkuu wa Tanzania baada ya kuchaguliwa na wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania.

Taarifa hiyo ya Ikulu inabainisha kwamba Zuwena Jiri amehamishwa kutoka mkoa wa Pwani kwenda kuwa katibu tawala mkoa wa Lindi akichukua nafasi ya Ngussa Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Samike alikuwa Katibu wa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na baada ya kufariki Machi 17, 2021, aliteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa wa Mwanza kabla ya kuhamishiwa mkoa wa Lindi.

“Viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mpya watajulishwa tarehe ya kuapishwa,” inaeleza taarifa hiyo iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Post a Comment

0 Comments