Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba SC, Azam FC, Young Africa zakwepana ASFC

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


 

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Shirikishso Tanzania Bara ‘ASFC’ Young Africans wamepangwa kucheza dhidi ya Geita Gold FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Michuano hiyo msimu huu 2022/23.


Young Africans ambayo ilitwaa ubingwa wa michauno hiyo msimu uliopita kwa kuifunga Coastal Union kwa changamoto ya mikwaju ya Penati baada ya sare ya 3-3 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid-Arusha, itacheza mchezo huo wa Robo Fainali nyumbani jijini Dar es salaam.


Geita Gold FC watakuwa na kazi kubwa ya kulipa kisasi dhidi ya Wananchi, hasa ikizingatiwa mwishoni mwa juma lililopita ilikubali kichapo cha 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Harry Kane kuzichonganisha Spurs, Man Utd

Mbali na mchezo huo wa Ligi Kuu, Geita Gold FC itakuwa inakumbuka mchezo wa Robo Fainali wa ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam msimu uliopita 2021/22. Mchezo huo ulishuhudia Geita Gold FC ikipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.


Meneja Arsenal amtahadharisha Gabriel Jesus

Michezo mingine ya Robo Fainali ya ASFC iliyopangwa leo Jumatano (Machi 15) kupitia Droo iliyofanyika Studio za Azam Media jijini Dar es salaam.


Simba SC 🆚 Ihefu SC


Singida Big Stars 🆚 Mbeya City


Azam FC 🆚 Mtibwa Sugar

Post a Comment

0 Comments