Stan Bakora Ashutumiwa Kumtelekeza Baba yake Mzazi Anayeokota Makopo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Stan Bakora ampuuza na kumtelekeza baba yake mzazi anayeokota makopo baada ya kutojali malezi yake tangu akiwa mtoto mchanga

Baba mzazi wa Mchekeshaji na Mtangazaji wa Efm, Stan Bakora ameonekana na wakulungwa akiokota makopo na kupita kwenye maduka mbalimbali mjini Morogoro akiomba msaada wa pesa za matumizi.
Alipoulizwa kwanini anafanya hivyo ikiwa mtoto wake ni Staa mkubwa, baba huyo amesema Stan alishamtelekeza anamtumia elfu kumi kila baada ya miezi sita, yani kwa mwaka anatumiwa elfu 20 au hatuniwi kabisa.

Amesema anateseka sana kama hana watoto na siku ikitokea akikutana na mwanae huyo atampa maneno mazito ya kumlaani na amemtaka aache kutumia jina lake la ukoo atafute jina la baba yake anayemuhudumia.

Kwa upande wa Stan alipotafutwa kujibu tuhuma hizo nzito amesema ni kweli hamuhudumii baba yake na hana mpango wa kurejesha moyo wake kuanza kumuhudumia kwa kile alichodai kwamba alimtelekeza tangu akiwa na mwaka mmoja na mtu ambaye anastahili kutumiwa pesa za matumizi ni bibi yake ambaye alifariki mwaka jana maana huyo ndiye aliyemlea na kumtoa kwenye mateso ambapo akiwa na mwaka mmoja tu baba yake alikuwa anamnywesha pombe.

Amesema baba yake alimtelekeza akaikimbia familia na kwenda nje ya nchi, na kwa huruma tu ikitokea akiomba chakula atampa lakini siyo kumpa pesa zake maana baba yake ana vituvitu ambavyo havizungumziki mbele ya umma ili kumstiri
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad