Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko ya vituo kwa mabalozi wawili na uteuzi wa balozi mmoja leo Aprili 3, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Unus, Rais Samia amempangia Balozi Humphrey Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu, Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.
Pia, amemteua Balozi Lt Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Mwisho, Rais Samia amemteua Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia nchini Uturuki. Kabla ya uteuzi huu, Bakari alikuwa Konseli Mkuu nchini Dubai.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, tarehe ya uapisho itatangazwa baadaye