Eng. Hersi Afunguka Kuhusu Kocha Nabi Kuondoka 'Offer Nyingi Zimekuja Lakini'

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Rais wa Klqbu ya Yanga, Eng. Hersi Said amewatoa hofu mashabiki wote wa Yanga duniani kote kuwa wanatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Mohamed Nasreddine Nabi.

"Sisi kama viongozi hatupo tayari kuona kocha yoyote ambaye yupo Kwenye benchi letu la ufundi anaondoka kwa sasa, tunaendelea kuijenga Yanga imara kwa sasa.

"Bado tuna malengo,,mipango endelevu na Kocha Nabi hivyo hatoweza kuondoka kwa gharama yoyote licha ya ofa nyingi zipo mezani kwetu kumuhitaji kocha wetu Nabi.

"Wananchi hawapaswi kuwa na woga wowote Nabi ataendelea kuwepo Yanga. Tupo ukiongoni kumaliza mashindano ya ndani Kama Ligi kuu NBC na Kombe la FA na kimataifa tupo hatua nzuri kwenda fainali.

"Kila siku sisi Kama Viongozi tunakumbushana majukumu yetu pamoja na wachezaji wetu wote ambao tupo nao kambini zawadi kubwa pekee kwa mashabiki wetu ni kuwapa ubingwa tu hakuna kingine.


"Bado ni mapema kuzungumzia usajili kuelekea msimu ujao ila kwa sasa tunamalizana kwanza na wachezaji wetu wote ambao kocha anataka kuendelea nao. Ila msimu ujao hatutafanya usajili mkubwa sana ila wachezaji ambao watakuja watakuwa wazuri kuja kuisaidia Yanga.

"Hili naomba Wanayanga wote wajue ni deni kwangu Kama ahadi yangu kwao, nitakuwa sina cha kujibu mbele za Mungu Kama nitashindwa kutimiza ahadi hii.

"Malengo yetu ya uwanja yapo palepale na ndani ya mwaka huu nyie wenyewe mtaanza kuona siwezi kuwambia ni lini ila ndani ya mwaka huu tutaanza utekelezaji huu wa uwanja wetu pale Jangwani, " amesemaEng Hersi.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad