Nabi Vs Kaizer Chiefs |
Baada ya Kukosa Dili la Kaizer Chiefs, Kocha Nabi Apagawa..Ashikwa Kigugumizi Kuzungumza
Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini imemteua Molefi Ntseki kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo.
Kaizer Chiefs ilikuwa ikihusishwa kumtaka aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nsreddine Nabi.
Kwa utambulisho huo wa Molefi Ntseki kuwa Kocha wa Kaizer ni dhahiri kuwa Kocha Nabi bado yupo sokoni.
NABI APATWA KIGUGIMZI.
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa hawezi kuzungumzia sababu iliyokwamisha dili lake na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
“Siwezi kutoa maelezo, kwa heshima ya Kaizer Chiefs. Sitaki kuzungumza kuhusu tatizo ni nini katika mazungumzo. Samahani kwa hilo,” Kocha, Nasreddine Nabi ameiambia #SundayTimes.
Nabi aliachana na Yanga baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiwa ameipa timu hiyo Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Ngao ya Jamii, lakini akiwa ameifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kaizer Chiefs imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamhitaji kocha huyo, jana akihojiwa na gazeti maarufu la Afrika Kusini, The South Afrika alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 wangekuwa wameshamalizana.
Kwa sasa Nabi yupo nchini Tunisia kulingana na vyanzo mbalimbali, wakati wakala wake yupo kwenye mazungumzo na Kaizer Chiefs kuhusu nafasi ya kocha mkuu.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA