Kaizer Chiefs kumng'oa Kocha Nabi Yanga

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Kaizer Chiefs kumng'oa Kocha Nabi Yanga

Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika kusini inafanya mazungumzo na Klabu ya pamoja na kocha wao, Nassredine Nabi kawa wataweza kumsaijili kuelekea msimu ujao.


Chiefs walimaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu ya DStv nchini Afrika Kusini (PSL) wakati wa kampeni za 2022/23 ambazo zimemalizika hivi karibuni pointi 26 nyuma ya mabingwa Mamelodi Sundowns.


Kaizer Chiefs hawajashinda taji lolote kuu tangu Mei 2015 na wamekuwa na makocha sita tofauti tangu Stuart Baxter alishinda ligi kuu nchini South Afrika kabla ya mkataba wake kumalizika.


Hivi karibuni Nabi alishinda taji la Ligi Kuu nchini Tanzania akiwa na Yanga kaa mara ya pili mfululizo na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo walipoteza kwa USM Alger kwa mikondo miwili mapema mwezi huu.


Kulingana na taarifa zaidi zilizotolewa kwa shirika la utangazaji la MSN na mtandao maarufu wa soka wa Goal.Com, zimesema kuwa si Kaizer Chiefs pekee, bali Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns wanamnyemelea Nabi kutaka huduma yake.


Raia huyo wa Tunisia mwenye umri wa miaka 57 hivi karibuni atamaliza mkataba wake na Yanga bado haijamfunga Nabi kwa mkataba mpya, na ule ambao alisaini mwanzoni alipofika Aprili 2021 unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Julai.


Ina maana iwapo Chiefs wataendelea na mazungumzo ya kumteua kama kocha wao ajaye, Nabi anaweza kujiuzulu mara moja na huenda akaondoka na wachezaji wake pendwa akiwemo straika Fiston Mayele raia wa Congo ambaye naye anatajwa huenda akaondoka Jangwani.


_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad