Ripoti ya Tume: Kifo Cha Mwanafunzi Nusura wa UDOM Hakihusiani na Ajali ya Waziri Dugange

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (#THBUB) imesema kifo cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nusura Hassan Abdallah kilitokana na shambulio kali la kupanda kwa Sukari na upungufu wa Damu

Kifo cha Nusura kilihusishwa na Ajali ya gari iliyomhusu Dkt. Festo John Dugange ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - OR, TAMISEMI (Afya)

Tume imeeleza ajali ya Dkt. Dugange ilitokea usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023 wakati Aprili 27, 2023 Nusura alisafiri kuelekea Moshi akiwa mzima wa Afya kabla ya kukutwa na mauti Mei 1, 2023 akiwa Hospitali alipokuwa akitibiwa baada ya kumaliza kula na kuanza kuumwa

Ripoti imeeleza mabaki ya chakula walichokula Marehemu Nusura, mchumba wake na mpwa wa mchumba wake; na matapishi yaliwasilishwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi ulionesha kutoonekana kwa dalili yoyote ya kuwemo kwa sumu

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad