Ukweli Kuhusu Benchi la Ufundi wa Yanga Kuondoka

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Ukweli Kuhusu Benchi la Ufundi wa Yanga Kuondoka
Ni kweli bench zima la Ufundi la Yanga lilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja tu, huku yote ikiwa imetamatika jana baada ya msimu wa kimashindano, ikiwa rasmi sasa wapo huru.

- Taarifa za uhakika ni kuwa Viongozi wa Yanga walishawaita na kuwapa ofa zao za kusalia klabuni hapo huku mpira upo kwa bench hilo sasa kuamua kwa mujibu wa ofa zao na ofa za Yanga mezani.

- Yanga kwa mujibu wa taarifa ni kuwa endapo bench litakuwa na mahitaji makubwa zaidi kuzidi ambacho kinaweza kupatikana basi watawapa mkono wa kwaheri na Yanga kuanza upya.

- Kocha Nabi ana ofa zaidi ya mbili ikiwemo ya Afrika Kusini huku Coacha Kaze ana ofa kutoka Singida Big Stars, wakati huo Kocha wa Makipa Nienov Milton anatajwa kutaka kwenda kuwa Kocha Mkuu sehemu nyingine.

- Yanga wana ofa yao na wao wana ofa zao, kinachosubiriwa ni kama watakutana hapo kati.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad