Mashabi wa USM Alger Waifanyia Vurugu Yanga Hotelini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya Yanga kushuka Uwanjani leo June 3 kumalizana na wenyeji wao USM Alger kundi kubwa la mashabiki wa Waarabu hao wamevamia hoteli ya Yanga na kufanya vurugu.

Mashabiki wa USM Alger usiku wa kuamkia Leo wamevamia hoteli ya Legacy ambayo kikosi cha Yanga kimeweka Kambi na kuanza kuimba nyimbo zao kwa dakika 16.

Hawakuishia kuimba peke yake mashabiki hao kabla ya kuondoka walipiga fataki za kutosha mbele ya hoteli hiyo kabla ya baadaye kutawanywa na walinzi wa hoteli hiyo.

Tayari uongozi wa Yanga umesharipoti matukio hayo kwa maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakiambatanisha na picha za video za matukio hayo.

"Tumeshawasiliana na watu wa CAF kuwapa hizi taarifa,kikosi kipo salama tulihakikisha hizi vurugu zao haziwaathiri wachezaji ingawa baadhi waliamka,"amesema bosi mmoja wa juu wa Yanga

Yanga itashuka uwanja wa ugenini Leo ikihitajj ushindi wa kuanzia mabao 2-0 dhidi ya USM Alger katika Fainali ya mkondo wa pili baada ya timu kupoteza nyumbani kwa mabao 2-1 hapa jijini Dar es Salaam.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad