Mtumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa auawa kikatili nyumbani kwake

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa





Mtu mmoja aliyefahamika kwa Merisiana Temu (42) mtumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ameuawa kwa kukatwa sehemu ya shingoni nyumbani kwake mtaa wa Mamboya Manzese kata ya Mkwatani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro.

 Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba amesema,taarifa za kuuawa kwa mtumishi huyo walizipata majira ya saa nne usiku Julai 17 mwaka huu  baada  siku hiyo kutoonekana kazini bila ruhusa na simu yake ikiwa haipatikani 

  Mabuba  amesema baada ya kutoonekana kazini Julai 17 mwaka huu ndipo watumishi wenzake  majira usiku walifika nyumbani kwake  kwa lengo kufuatilia kujua kilichomsibu marehemu kutofika kazini ndipo walikuta mlango ukiwa wazi na funguo zipo kwa ndani na walipoingia sebuleni wakakuta amelala chini damu nyingi zikiwa zimemwagika chini huku akiwa na majeraha sehemu mbalimbali

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa Morogoro ACP Hassan Omary ,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema marehemu alikua akiishi peke yake hadi sasa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika huku Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi  na kusisitiza kamati ya ulinzi na usalama kuendelea kuchunguza aliyehusika na tukio hilo

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad