Watu watano wanusurika kifo Morogoro, dereva wa basi ashikiliwa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshilikia Fauzi Abasi Dereva wa Basi Kampuni ya Ester yenye namba za usajiri T 279 DZX baada ya Dereva huyo kuonga Pikipiki ya magurudumu matatu katika eneo la Kihonda Mbuyuni Barabara kuu ya Morogoro - Dodom na kusababisha watu watano kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hasaan Omary amethibitisha kutokea kwa ajaili hiyo ambapo amesema chanzo ni Dereva wa Basi kutaka kupita magari mengine bila ya kuchua tahadhari.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Abilah Issa amesema wamepokea Majeruhi watao wa wakiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wengine wamevunjika mifupa,pamoja na maumivu ya kifua.

Kwa upande wao Majeruhi na Mashuhuda wa Ajali hiyo wamesema imetokea majira ya saa3 asubihi ikihusisha Basi la Kampuni ya Ester ikitokea Jiji Dar es Salaam kuelekea Singinda na Bajaji iliyokuwa na watu watano ikitokea Makunganya kuelekea Morogoro mjini.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad