Haya Hapa Matokeo Yanga Vs Namungo Leo September 20, NBC premier League

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Haya Hapa Matokeo Yanga Vs Namungo Leo September 20, NBC premier League

Haya Hapa Matokeo Yanga Vs Namungo Leo September 20, NBC premier League


Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa uwanja wa Azam Complex kuikaribisha Namungo Fc

MATOKEO

YANGA 1:0 NAMUNGO

Wafungaji:

Mudathiri

Ni mchezo wa raundi ya tatu Yanga ikiwania alama tatu ambazo zinaweza kuwarejesha kileleni mwa msimamo wa ligi

Bila shaka utakuwa mchezo wenye ushindani kwani unazikutanisha timu ambazo katika misimu ya karibuni zimekuwa na upinzani mkali

Yanga wameanza vyema ligi msimu huu wakishinda mechi zote mbili walizocheza huku wakipachika mabao 10 bila ya kuruhusu bao

Namungo Fc wao walianza ligi kwa kuchechemea kwani licha ya kuanzia nyumbani katika mechi zao mbili, waliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC huku wakichapwa bao 1-0 na JKT Tanzania

Namungo Fc inanolewa na kocha Cedric Kaze ambaye amewahi kuwa kocha mkuu na baadae kocha msaidizi wa Yanga

Katika mkutano na wanahabari jana Kaze alitamba kuwa licha ya ubora wa Yanga yapo madhaifu ambayo yeye leo atayatumia kuhakikisha timu yake inapata matokeo mazuri

Kuelekea mchezo huo Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi alidokeza kuwa kikosi chake kinaweza kuwa na mabadiliko katika baadhi ya maeneo kwa kuzingatia mahitaji ya mchezo huo

Yanga ilicheza mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh siku ya Jumamosi nchini Rwanda na kikosi kilirejea jijini Dar es salaam siku ya Jumatat

Gamondi alisema wapo wachezaji walipata majeraha madogo madogo huku wengine wakikabiliwa na uchovu hivyo atatumia wachezaji ambao watakuwa tayari kwa mchezo huo

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad