Rais Samia Apongeza Tanzania Kuandaa AFCON 2027
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na kitendo cha Tanzania kuwa sehemu ya waandaaji wa Mashindano ya AFCON 2027 ikiwa pamoja na Mataifa ya Kenya na Uganda.
Shirikisho la Soka Afrika CAF limetoa uenyeji wa nchi hizo za East Afrika kuandaa michuano hiyo mikubwa.
Rais Samia aliandika “ Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda. Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu.
"Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma," aliandika Rais Samia.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA