Header Ads Widget


Ruby "Kusah Ndiyo Mtu wa Kwanza Kunipeleka kwa Mganga"

 

Ruby "Kusah Ndiyo Mtu wa Kwanza Kunipeleka kwa Mganga"

Kupitia Mashamsham ya Wasafi FM, Msanii wa kike Ruby amesema awali hakuwahi kumjua Mganga wala ndumba zinafanywaje, lakini baada ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mzazi mwenzie Kusah ambaye pia ni Msanii wa muziki wa Bongo Flava, alimpeleka kwa Mganga mara yake ya kwanza katika maisha yake.


Ruby amesema anaamini Kusah alimroga ili wasiachane lakini nguvu ya Mungu ilizidi uwezo wakafanikiwa kuachana na akaacha kuisujudia ndumba. Ameongeza kuwa licha ya kupata Mtoto pamoja lakini Kusah hatoi matumizi kwa Mtoto huyo na mara ya mwisho kumuona ilikuwa kabla hawajaachana.


Amesema yeye ndiye aliyemtambulisha Kusah na kumleta mjini, ambapo alikuwa anamshirikisha kwenye nyimbo kadhaa na kumuombea "show" ili aweze kufahamika. Licha ya kuachana Ruby amesema Kusah amekuwa akimsumbua mara kadhaa.

Post a Comment

0 Comments