TAARIFA: Wachezaji wa Simba watakao ukosa mchezo wa Power Dynamos ligi ya Mabingwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mohbad alifikishwa hospitali akiwa amefariki tayari, hospitali yakanusha taarifa za awali!


TAARIFA: Wachezaji wa Simba watakao ukosa mchezo wa Power Dynamos ligi ya Mabingwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji watatu wataukosa mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamo

Mchezo huo utapigwa Jumapili, Oktoba 1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Ahmed amesema beki Hennock Inonga bado anaendelea kuuguza jeraha alilopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji

Ahmed pia amewataja mlinda lango Aishi Manula ambaye bado anaendelea kuimarika wakati Aubin Kramo hayuko tayari kutumika kwenye mechi ya ushindani kwani kuwa bado hajapona sawasawa majerah


"Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki timu ilirejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Power Dynamos"

"Mpaka sasa ni wachezaji watatu (Inonga, Kramo, Manula) ambao tuna uhakika wataukosa mchezo lakini wachezaji wengine wote wanaendelea na maandalizi"


"Tunatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki ili kuwaweka sawa wachezaji kuelekea mchezo husika. Ni takribani siku 9 wachezaji hawatakuwa na mechi yoyote kitaalamu hili sio jambo zuri kuelekea mchezo muhimu ambao tunahitaji matokeo mazuri ili kutinga hatua ya makundi," alisema Ahmed-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad