Yanga waichapa Tabora United ugenini, Aziz KI akitaka kiatu Mfungaji Bora
Mabingwa watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, makao makuu ya nchi.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 21 na kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 11, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
Tabora United baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 15 za mechi 13 sasa nafasi ya 12 kwenye ligi inayoshirikisha timu 16 za mikoa 11.
Hili ni bao la 10 kwa Aziz KI akiwa anaongoza katika orodha ya wafungaji wa magoli Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA