Simba imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi 2024 baada ya kulazimishwa suluhu na moja ya timu wageni walikwa kwenye mashindano hayo APR ya Rwanda.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha alama 7 ikishinda mechi mbili na kutoa sare ya Leo ambapo sasa itakutana na Jamhuri ya Pemba katika hatua ya robo fainali.
Jamhuri itakwenda kukutana na Simba ikikumbuka kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Yanga kwenye hatua ya makundi.
Kocha wa Simba Abdelhak Benchikha amebadili kikosi karibu kizima lakini bado kilikuwa na ubora wa kumiliki mchezo wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga.
APR ambayo ni timu ya jeshi nayo ilikuwa na matukio ya kupata mabao lakini utulivu wa wachezaji ukashindwa kuipa matokeo timu hiyo.
Licha ya Benchikha kufanya mabadiliko kipindi cha pili akiwaingiza baadhi ya mastaa wake wakiwemo Willy Onana, Luis Miquissone na Mosses Phiri bado wekundu hao wakashindwa kubadili ubao wa mabao.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuongoza kundi lao wakifikisha alama 7 huku Singida Fountain Gate ikiwa nafasi ya pili na alama 6 huku APR ikiwa ya tatu na alama zao 4 na kujihakikishia nafasi ya mshindani Bora.
APR sasa itakutana na Yanga kwenye hatua ya robo fainali kwa mechi zitakazoanza Januari 7.
RATIBA ROBO FAINALI
– KVZ vs Mlandege FC (Januari 7 saa 10:15 jioni)
– Yanga SC vs APR FC (Januari 7 saa 2:15 usiku)
– Azam FC vs Singida FG (Januari 8, saa 10:15 jioni)
– Simba SC vs Jamhuri SC (Januari 8, saa 2:15 usiku)
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA