Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Muhene "Try Again" ametangaza kujiuzulu wadhifa huo katika Klabu ya Simba leo Juni 11, 2024.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya wajumbe kadhaa kutangaza kuachia ngazi huku yeye ikisemekana kuwa amegoma kung'atuka madarakani.
Try Again amemuomba mwekezaji ndani ya Simba Mohammed Dewji kurejea na kuchukua wadhifa huo kwa ajili ya maendeleo ya Simba SC huku yeye akibaki kuwa Mwanachama wa kawaida.
Akizungumza Try again kupitia televisheni amesema;
“Kwa maslahi mapana ya Simba kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimemwomba Mwekezaji wetu Mohamed Dewji MO arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama Mwanachama na Kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba, kwa maana hiyo natangaza kuondoka kwenye kiti
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA