FIFA: Hii hapa orodha mpya ya timu bora za soka Duniani
Mabingwa wapya wa bara Ulaya, Uhispania wamepanda hadi nafasi ya tatu katika viwango vya hivi punde vya FIFA vilivyochapishwa Alhamisi.
Washindi wa kombe la dunia 2022, Argentina wakishika nafasi ya kwanza kufuatia ushindi wao wa Copa America.
Viwango hivi vinakuja baada ya mwezi wa shughuli nyingi za soka, huku Argentina ikiishinda Colombia na kutwaa taji la Copa America na Uhispania ikiishinda Uingereza na kutwaa ubingwa wa Ulaya.
England ilipanda hadi nafasi ya nne, na kuruka Brazil ambao walionyesha viwango vya chini kwenye mashindano ya Copa America.Brazil walibanduliwa na Uruguay kwenye robo fainali baada ya mashuti ya penalti.
Kwingineko katika hatua ya 50 bora, timu mbili zimepanda daraja kwa njia ya kuvutia baada ya kutinga robo fainali ya mashindano yao ya bara.
Uturuki imepanda kutoka 42 hadi 26 na Venezuela ikipanda hadi nafasi ya 37 kutoka 54.
New Zealand wamepanda hadi nafasi ya 94, wakirejea miongoni mwa 100 bora baada ya kushinda kombe la OFC.
Tazama orodha ya kumi bora:
1. Argentina
2. Ufaransa
3. Uhispania
4. Uingereza
5. Brazil
6. Ubelgiji
7. Uholanzi
8. Ureno
9. Kolombia
10. Italia.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA