Msemaji wa Klabu ya Yanga Sc, Haji Manara leo Julai 22, 2024 amezungumza na waandishi wa habari akitoa shukrani kwa wadau mbalimbali wa soka waliokuwa pamoja nae kwa kipindi chote alichokuwa akitumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili.
Manara ambaye amemaliza adhabu yake aliyofungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi, adhabu ya miaka miwili pamoja na faini ya milioni 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema licha ya kuwa nje ya ofisi lakini waajiri wake wamemuongezea mkataba na mshahara.
Manara aliyekuwa ameambatana na familia yake kwenye kikao hicho amesema sambamba na kutumikia 'kifungo cha soka' cha miaka miwili pia amelipa faini ya shilingi milioni 10 za Tanzania iliyokuwa imeambatanishwa kama sehemu ya adhabu yake.
“Mkataba wangu na Yanga SC ulikuwa unaisha 2025, lakini GSM waliniita na kuniongeza mkataba mpya ambao unaisha 2026, nilishangaa maana nilikuwa sifanyi kazi. Lakini nimeongezwa mkataba na nimeongezewa mshahara. Namshukuru sana Ghalib, licha ya kufungiwa nilikuwa naendelea kulipwa mshahara," amesema Manara.
Aidha, Manara amethibitisha rasmi kushiriki katika matukio yote ya Yanga ikiwemo uzinduzi wa jezi na siku ya Mwananchi.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA