Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Haji Manara akizungumza na wanahabari leo, Jumatatu Julai 22.2024 Serena Hotel, jijini Dar es Salaam amesema adhabu yake ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili (2) iliyokuwa imetolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) imemalizika rasmi jana, Jumapili Julai 21.2024 hivyo kwa sasa yuko huru kuendelea na majukumu yake kama mwajiriwa wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) kama Msemaji wa klabu hiyo
Manara aliyekuwa ameambatana na familia yake kwenye kikao hicho amesema sambamba na kutumikia 'kifungo cha soka' cha miaka miwili pia amelipa faini ya shilingi milioni 10 za Tanzania iliyokuwa imeambatanishwa kama sehemu ya adhabu yake
Alipoulizwa ni kwa jinsi gani atakwenda kufanya kazi klabuni hapo ikizingatiwa kuwa majukumu anayokusudia kwenda kufanya kwa sasa yanafanywa na Ali Kamwe (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC) Manara amejibu kuwa yeye ndiye msemaji wa Yanga SC na kwamba kabla hajafungiwa amefanya kazi kwa takribani mwaka mmoja (1) na Hassan Bumbuli (Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC) bila kuingiliana kwenye majukumu kwa kuwa kila mtu alifanya majukumu yake, hivyo ni matumaini yake kuwa hata kwa waliopo sasa itakuwa hivyo
Manara amekanusha madai ya kuwa Ali Kamwe ni 'Boss' wake badala yake ameendelea kutoa msisitizo kwa wanahabari na Watanzania kwa ujumla kufahamu kuwa wawili (2) hao kila mmoja anatimiza majukumu yake
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA