Hatimaye Muna LOVE Ajifungua Mtoto wa kiume

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Hatimaye Muna LOVE Ajifungua Mtoto wa kiume

Staa wa kitambo kunako anga la Bongo Muvi, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amejifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Testmony.


Muna ambaye aliwahi kuwa na mtoto wa kiume aliyefahamikwa kwa jina la Patrick ambaye alifariki mwaka 2018, kupitia ukurasa wa Instagram ameposti picha yake akiwa na kichanga chake na kusindikiza na ujumbe huu:


Asante YESU kwa kunirudishia zaidi ya kile ulichochukua, nikisema nianze kuelezea matendo yako makuu juu yangu sitamaliza. Walinipiga fimbo nyingi za maumivu, maneno ya kejeli na kila walichoona nastahili.


Lakini sikuchoka neno langu lilikuwa wakati nalia kwa uchungu ndani ikiwa mbele zao najikaza najifanya siumii nilikuwa nakuambia kwa uchungu wewe YESU unajua ukweli unanijua niponye, wewe YESU unaona naomba tu niponye uchungu huu, haya maneno leo najivunia. YESU ASANTE.


Nilikuahidi kuwa ukinipa mtoto yeyote tena nikakuomba arudi tu kama yule atafanya kazi yako kwa Dini zote na nitakutangaza kama chizi nitasimulia Matendo yako Makuu bila aibu, nitajivunia wewe popote na hata sasa UMEJIBU MAKUBALIANO YETU . YESU ASANTE.


YESU kama ulivyonipa, nakuomba unajua kukutangaza wewe ni vita, namfunika mwanangu kwa damu yako Takatifu, atakayemgusa au kumnenea mabaya akakutane na Wewe.


Mimi siwezi zuia chochote Baba yangu, ile ahadi niliyokuahidi nitafanya hapa hapa, walikonikejeli na kunichapa fimbo za maneno nitawaonyesha Ukuu wako, najua unaona YESU ila ulinzi wako Baba kwa kuwa sehemu ni hii YESU NAMKABIDHI TESTMONY MIKONONI MWAKO .


YESU kakumbuke wale wahitaji waliokata tamaa na waliosubiri kwa muda mrefu.


Si kama mimi umenipendelea hapana bali wajaze IMANI kama ulivyonijaza na uwajibu kwa kuwapa uzao au kile wanachoomba na kustahili, ili waone Matendo Makuu juu yako.


PATRICK ninaimani umefurahi nisamehe kwa kukulaumu ni Uchungu na maumivu makali. YESU ASANTE KWA KUNIPA BABY BOY TENA


Kwa kuwa Maisha yangu na hii Baraka imekuja kama majibu ya maombi yangu basi ataitwa TESTMONY na JINA LINGINE LA MUSLIM NASUBIRI NTASEMA.


YESU AKUTUNZE BABA YANGU TESTIMONY, ukue tufanye kazi ya Bwana nakutabiria BARAKA, FURAHA , HUYU YESU AKUJAZE HEKIMA YA HUDUMA UKATANGAZE NENO LAKE

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad