Kitendo cha kuungo mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho kushinda kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu, kimeibua maswali na mijadala kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Tanzania.
Huu ni msimu wa tatu kwa Aucho ambaye ni raia wa Uganda tangu ajiunge na mabingwa hao wa Ligi kuu amekuwa akifanya vizuri lakini hatajwi kwenye orodha ya kushindania tuzo jambo ambalo limewaibua wadau wa soka na kuhoji nini kipo nyuma ya pazia kwa kamati inayoandaa tuzo hizo.
Baadhi ya Comments:
@wakanda_republic: "Kwa miaka yote mitatu ambayo Khalid Aucho ameitumikia ligi kuu Tanzania bara hajawahi kukakaa kwenye orodha ya watu wanaowania tuzo ya kiungo bora, nafikiri kuna sehemu ambayo TFF wametupunja kwenye majina ya wanaogombea hizi tuzo"
"Sisemi alistahili kushinda tuzo ya kiungo bora lakini kwangu mimi nina imani Kwa performance ambayo ameitoa msimu huu nafikiri alistahili kuwepo kwenye orodha ya kiungo bora."
@waziri_wa_wapwa; "Hivi Aucho imekuaje amekosekana hata kwenye nominees wa tuzo ya kiungo bora wa msimu,kwamba hastahili au?"
@lapulgajr_30: Wanao wania tuzo ya kiungo bora ⏩Stephane aziz ki ⏩Feisal salum abdallah ⏩Kipre Jr
⏺Msimu wa pili mfululizo khalid aucho hayupo na sio kwamba mpira tunausikiliza kwa redio hapana tunaona....nadhani TFF kuna namna huwa inakuwepo yaani Kipre over Khalid."
Haatim Abdul @Penaltytaker12: "Hata kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hajaingia? Sina shaka huyu ndio mchezaji aliepiga second assists nyingi zaidi kwenye ligi. Spotlight imebebwa na walio juu yake lakini mipira mingi ya hatari wameipokea kutoka kwa Khalid Aucho. Mechi mbili za ligi bila yake zote Yanga wamelose.
@MakabalaJoseph: "Hivi hii inaukwel!?? Wowote Ni msimu wa tatu mfululizo AUCHO hajaingia kwenye kuwania tuzo ya kiungo Bora wa ligi kuu.
@earadiofm: "Wachambuzi wengi wanasema Aucho ndio injini ya Yanga lakini kwenye Tuzo hatumuoni, kuna gap kubwa kati ya wachambuzi na waandaaji wa Tuzo.
@mchizidamas: "Kwenye miaka 3 ya Aucho ndani ya Yanga Sc hajawahi kuingia kwenye list ya tuzo za kiungo bora wa msimu achilia mbali kuchukua. Max last season in term of numbers au statistics zingine bado alisthili kuwa kwenye list,Yahya Zaid, Mudathar na Najim mussa hao wote walistahili."
@JamboTanzania1: "Kama vp wadau tumuandalie Aucho tuzo yake maana pale tff wameamua kumkazia mwana.
@iammwanjala: "TFF ya Karia Sijui inaangaliaga nini kwenye tuzo za Kiungo bora. Khalid Aucho kwa misimu yote mitatu aliyokaa Yanga alidesrve kuwa kiungo bora Ila ajabu hata kwenye list ya wanaogombea anakosekana!! Maajabu!.
@aggrey_sports: "Kitendo cha Kukosekana kwa AUCHO kwenye Tuzo za Tff ni dhahiri kabisaa uongozi haujui nini unataka kwenye tuzo hizo.
Unapozungumzia Kiungo mkabaji Kwenye ligi yetu ya NBCPL huwezi kusahau jina la Aucho, kiukweli nimeshangazwa na hiyo kamati ya upangaji wa tuzo."
@Mwacha5: "@aucho_khalid08 Wewe ni bora kuliko hizo tuzo zao CHAMA IS GREEN & YELLOW.
@Yangadiefan: "Klabu yetu impe huyu jamaa tuzo ya heshima @YoungAfricansSC."
@MarcoMzumbe: "Kamati ya tuzo kuna muda inabidi tu uielewe maana ukisema wamemsahau Maxi kwenye tuzo bado utajiuliza kuhusu Khalid Aucho wakati huo unakumbuka Mudathir Yahya na simu zake kakosekana, fikiria hata ungekuwa wewe kwenye kamati ungefanyaje."
@ramadhan_shamte: "AMEANDIKA KIUNGO WA YANGA KHALID AUCHO. Hakuna tuzo bora kuliko upendo wenu na support yenu. Mashabiki wangu wapendwa asanteni kila mara kwa kuniunga mkono tangu siku ya kwanza. Asante sana."
@ShabbyLove6: "Hata wasipo kupa mzee wa kazi ila sisi kazi yako ni zaid ya tuzo keep pushing."
@Mihambojunior1: "Nimefuatilia nominees wa hizi tuzo za NBCPL na nikapata yafuatayo: Tuzo ya mchezaji Bora wa msimu mzize kajumuishwa then Aucho, Pacome wote hawapo. For me nafikiri sio sawa, Athari ya Aucho na Pacome ni kubwa kuliko ya mzize. Kuhusu Mudathiri pia alistahili kuwepo."
@g_ki02: "@Tanfootball kwani kiungo bora kwenu mnataka aweje? Wachezaji wengi wa @YoungAfricansSC walistahili kuwepo kwenye hizi tuzo na hii nikwasababu wao walikuwa bora sana. Aucho, Max na Mudathir walistahili kushindania tuzo ya kiungo bora. Shwain."
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA