Mwanasheria wa Yanga "Kwa Kuwa Kibu Denis Hakuwa na Furaha Simba, Mwacheni ale Maisha Ulaya"

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa insta!
"Hizi changamoto za wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao ni matokeo ya ushabiki na wachambuzi wetu.

Kwa sasa, kuna wimbi la wachezaji kutoroka na wengine kuwa na mikataba na timu zaidi ya moja kwa madai kwamba hawana furaha na wanaenda kutafuta fursa bora zaidi.

Ushauri wangu kwa BMT ili kuokoa soka letu ni kuweka kanuni inayolazimisha mchezaji yeyote mwenye mkataba akihama kutoka klabu moja kwenda nyingine lazima kuwe na Mkataba wa Uhamisho (Transfer Agreement) au Mkataba wa Kusitisha kwa Pamoja (Mutual Termination Agreement) uliothibitishwa na BMT na kulipiwa ushuru wa stampu (Stamp Duty).

Mchezaji au timu yoyote ikikiuka, basi mchezaji huyo asipewe kibali cha kucheza nchini, period.

Bila hatua hiyo, migogoro ya wachezaji wenye mikataba haitaisha kamwe na TFF itaendelea kulalamikiwa bure.

NB: Kwakuwa tulishakubaliana kama mchezaji hana furaha aruhusiwe kuondoka, Rasta asiguswe acha ale maisha😂" @simon.esq
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad