Mzee Makamba Ampongeza Rais Samia Kuwatumbua Nape na January Makamba

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa




Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuf Makamba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi yake ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Januari Makamba.

Mzee Makamba ambaye ni nguli wa siasa nchini amesema uamuzi wa Rais ni katika kuimarisha safu ya timu yake ambayo itamsaidia kutekeleza Ilani ya Chama hicho ambayo amekabidhiwa.

“Kwanza ninampongeza rais (Samia Suluhu Hassan) kwa mabadiliko aliyofanya, pili ni kuwapongeza walioteuliwa, wafanye kazi ya kumsaidia rais na tatu ni kuwapongeza walioondolewa na wao wanastahili pongeze kwa sababu kwa kipindi chote walichomsaidia rais walijitahidi kwa uwezo wao wote, wanastahili pongezi.

“Rais ni kama kocha wa klabu ya soka, amekabidhiwa ilani ya chama na kukabidhiwa majukumu ya kuteua watu wa kumsaidia kutekeleza ilani hiyo. Yeye ndiyo anaamua nani amsaidie kazi hii na nani amsaidie kazi ile, akiona huyu ananifaa basi anamleta kwenye timu yake ili amsaidie.

“Kocha wa Simba akimtoa mchezaji una mlaumu? Mambo yanayoweza kusababisha akamtoa mchezaji ni kwamba huenda amechoka amekata pumzi lakini pumzi zikirudi atamrudisha tena maana hawa waliotoka walikuwemo wakatoka baadae wakarudi na leo wametoka tena, kwa hiyo usije ukashangaa baadae akawarudisha tena.

“Nasema rais ni kama kocha wa Yanga, hiyo jukumu lake ni kuhakikisha timu inapata magoli. Na hawa aliyowapumzisha sio kwamba hawajui kucheza pengine pumzi zimeisha lakini baadae akamwambia ingia tena,” amesema Mzee Makamba.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad