Prince Dube Aanza Kutupia Yanga ikiitungua TS Galaxy

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Prince Dube Aanza Kufunga Magoli

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya TS Galaxy ya Ligi Kuu nchini Afrika Kusini kwenye mechi ya kirafiki ya Mpumalanga Premier Cup iliyopigwa nchini humo.


Bao pekee la mshambuliaji mpya wa Yanga, Prince Dube alilofunga dakika ya 55 akitokea benchi, limetosha kuwapa Wananchi furaha mpaka kipenga cha mwisho cha mchezo huo.


Hili ni bao la kwanza kwa Dube ambaye ni raia wa Zimbabwe tangu ajiunge na Yanga akitokea Azam FC.


Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kwenye mashindano hayo baada ya ule wa kwanza, Yanga ilichezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa FC Augsburg ya nchini Ujerumani.


Mpaka sasa katika mechi mbili za kirafiki walizocheza nchini Afrika Kusini, Yanga wamefanikiwa kufunga magoli mawili ambayo yote yamefungwa na washambuliaji wapya, Baleke na Dube huku pia wakiruhusu magoli mawili.


Katika mchezo wa leo, Kocha Miguel Gamondi alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kilichoanza tofauti na kile dhidi ya Augsburg kwani kati ya wachezaji 11, watatu pekee Dickson Job, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Clement Mzize ndiyo wameanza.


Khalid Aucho na Denis Nkane ambao hawakuwepo kabisa katika mchezo wa kwanza leo wamepata nafasi ya kucheza.


Kikosi kilichoanza leo ni Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomary, Farid Mussa, Dickson Job, Aziz Andabwile, Jonas Mkude, Sure Boy, Mudathir Yahya, Clement Mzize, Shekhan Khamis na Denis Nkane.


Yanga itashuka tena dimbani Jumapili Julai 28, 2024 kuvaana na Kaizer Chiefs inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye ametua kwenye kikosi hicho msimu huu.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad