Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Hukumu ya kesi ya wanamuziki Soggy Doggy na Dataz dhidi ya Home Box Office (HBO) ya Marekani imesomwa leo Mahakama kuu ya Tanzania na wasanii hao kushinda kesi
Wasanii hao wakiwakilishwa na kampuni ya Markel Advocates walifungua kesi mahakamani hapo mwaka 2021 wakidai HBO kutumia wimbo wao wa "Sikutaki tena" kwenye filamu yao ya "Sometimes in April" iliyochezwa na staa Idris Elba bila ruhusa au makubaliano na wasanii hapo
Hatimaye leo wasanii hao wamepewa ushindi kwa kazi yao "kuibwa" na HBO wametakiwa kuwalipa zaidi ya shilingi milioni 700 na bado wana nafasi ya kukata rufaa.
Sikutaki tena ni wimbo ulioimbwa na Dataz akimshirikisha Soggy Doggy na ulitoka nwanzoni mwa Mwaka 2000 ukirekodiwa katika Studio za Soundcrafters chini ya mtayarishaji Enrico.
Wasanii hao wameishukuru Mahakama kwa kuona wanastahili haki na kuomba wasanii kutochukulia poa kazi zao.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA