Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Saa chache baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kutangaza kurejea katika majukumu aliyokuwa anafanya awali Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa baraka zote.
Manara jana alitangaza kurejea kazini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya TFF kupitia Ofisa Habari Clifforf Ndimbo amesema Manara yuko huru kuendelea na majukumu yake baada ya kukamilika kwa adhabu.
Ndimbo amesema mbali na Manara kumaliza adhabu pia amelipa kiasi cha sh 10 Milioni ikiwa ni faini iliyoambatana na kifungo hicho.
“Manara yuko huru kweli na hata huo mkutano alioufanya hajakosea kitu kwa kuwa hajafanya kosa lolote kikanuni adhabu yake ilimalizika” amesema Ndimbo.
“Ukiachana kumalizika kwa adhabu hiyo kutokana kudaiwa kufanya makosa ya kimaadili alipowaruzana na Rais wa TFF Wallace Karia katika Fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal UNion ya Tanga uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid JIjini Arusha.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA