Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Kipre Jr |
Timu ya Azam Yaendelea Kubomoka, Kipre Jr Akimbilia USM Algier
Klabu ya Mouloudia Club d'Alger, maarufu kama MC Alger ama MCA ya Algeria imekamilisha usajili wa aliyekuwa winga wa Azam Fc, Kipré Zunon Junior Kaa.
Azam imetangaza kumuuza Kipre Junior kwenda kwa Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Algeria wamempa Kipre mkataba wa miaka minne utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2028.
Azam Fc itapokea kitita cha dola 300,000 (takribani milioni 797) kwa mauzo ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ivory Coast.
Msimu uliopita, nyota huyo alifunga magoli tisa (9) na kutoa assist tisa (9) kwenye mechi 28 alizocheza za NBC Premier League akitumia dakika 1630 akiwa na uzi wa Azam FC.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA