Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmedy Ally amethibitisha kuwa Kibu Denis amerejea kikosini na amezungumza na kumalizana na Kocha Fadlu Davids, hivyo mambo yapo sawa.
Ahmedy pia amesema Simba itamchukulia hatua za kinidhamu Kibu ili asirudie na iwe funzo kwawengine.
“Kibu Denis amerejea Dar es Salaam (Akitokea Norway) atakuwepo Simba day, klabu imemsamehe ila lazima impe ADHABU kutokana na utovu wa nidhamu,” amesema Ahmed Ally.
Wkati Kibu Denis ametorokea Norway alipoitwa kufanya majaribio na timu ya Ubelgiji, Ahmed Ally alifunguka jinsi usajili wa mchezaji huyo, ulivyoisumbua klabu katika kumuongeza mkataba.
“Hakuna usajili uliotutesa Simba kama wa kumuongezea mkataba Kibu Denis. Alikuwa anasema ntaongeza mkataba, ntaongeza mkataba Anapitia huku anatokea huku. Wavimba macho nao walikuwa wanamvizia Hatukulala wiki mbili.
“Watu wanasema ana goli moja. Ndio ana goli moja lakini anajituma sana. Kibu ni aina ya wachezaji ambao wanacheza kama timu za baba zao, Hakuna timu inatamani kukutana na Kibu,” amesema Ahmed Ally.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA