Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Klabu ya Simba Sc imemtangaza nyanda Moussa Pinpin Camara kama mchezaji mpya
Klabu ya Simba Sc imemtangaza nyanda Moussa Pinpin Camara kama mchezaji mpya
Klabu ya Simba imemtangaza nyanda Moussa Pinpin Camara kama mchezaji mpya klabuni hapo akitokea klabu ya Horoya AC ya Guinea.
Camara (25) raia wa Guinea mwenye urefu wa sentimita 185 amesaini mkataba wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2026 na tayari yupo Benjamin Mkapa kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kuelekea Simba Day hapo kesho.
Mpaka sasa Klabu ya Simba ina magolikipa watano Ayoub Lakred, Hussein Abel, Ally Salim, na Camara japokuwa mustakabali wa Aishi Manula Klabuni hapo bado haujajulikana.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA