Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
BREAKING: Yanga Yashinda KESI Dhidi ya Magoma
Leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwa ni siku ya hukumu katika kesi ya Yanga na Juma Ally Magoma ikumbukwe kwamba siku ya Jumatano ndiyo ilipangwa kesi hiyo kutolewa hukumu lakini wakili wa Mzee Juma Ally Magoma na Geofrey Mwaipopo hakutokea mahakamani na kufanya kesi kuahirishwa hadi siku ya ijumaa tarehe 9 August 2024.
KUR JUAN IMEMRUDIA MAGOMA
Mzee Magoma ameshindwa kwenye kesi yake dhidi ya Yanga ambapo hukumu imetoka leo Agosti 9, 2024 saa 5 asubuh katika mahakama ya kisutu na anatakiwa kuilipa fidia klabu ya Yanga.
Akizungumza na Wasafi Media, Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe amesema kuwa, Magoma ametakiwa kuilipa Yanga gharama zote walizotumia katika kuendesha Kesi hiyo.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA