Baada ya baadhi ya mashabiki kudai kuwa msanii wa bongo fleva, Harmonize hakufanya vyema tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi ‘Yanga Day’.
Harmonize ameamua kutoa maelezo haya kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa insta story kwa kusema kuwa:
“Kwa yeyote alie zungumza kuhusu show yangu Yanga Day kuwa nzuri au mbaya kumbuka its Konde vs Konde. Uzuri hawasemi nani kafanya vizuri zaidi anyway kwa akili ya kawaida tu ni wazi kwamba wanaifananisha hii na ile Yanga Day niliyoingia na kamba asanteni kwa kuendelea kutunza hizo kumbukumbu vichwaniii!!! Inanifurahisha na inanipa faraja kwamba nilifanya kitu kizuri that day!!!”
“Simba & Yanga ni team kubwa sanaa zenye mashabiki wengi matamasha haya yenye mvuto mkubwa kufanyika siku mbili zilizo ongozana yaani Simba Jumamosi, Yanga Jumaapili lazima kuwe na ugumu.
“Binafsi nimekabidhiwa uwanja saa nane usiku Jumamosi baada ya Simba kumaliza tukio lao. Thank you God tumefanya the best we can do mashabiki wa Yanga wote asanteni kwa support.
“Hakika nyinyi ni familia!!!! Bila shaka tume enjoy sanaa sikukuu yetuu uongozi team nzima ya Yanga asanteni kwa kuendelea kuniamini na kunipa nafasi !!! Next time will be more yess we made biggest song #YangaBingwa,” ameandika Harmonize.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA