SIYO RAHISI NA HAIWEZEKANI KUWA JAMBO LA SIRI...!
Nimeona mjadala wa kuhusu kurejea kwa Wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wa CHADEMA Kurejea tena ndani ya CHADEMA.
lakini katika hali ya taharuki na sintofahamu siyo tu kwa Viongozi wakubwa wa CHADEMA bali hata viongozi wa wilaya na mikoa wa CHADEMA na wao wameonekana kushangazwa na habari hii wakiwa wameshtushwa na jambo hili. kwamba imekuwaje wamerudi..?
Lakini pia kuna propaganda kutoka ndani na nje ya CHADEMA za kuaminisha wanachama na Wananchi kuwa akina Mdee wamesharejea tayari ndani ya CHADEMA na kwamba mchakato huo wa kuwarejesha Wabunge hao umefanywa kwa mapenzi ya baadhi ya Viongozi fulani.
USAHIHI
Kwa kumbukumbu sahihi ndani ya CHADEMA hadi wakati huu,Wabunge 19 siyo wanachama wa CHADEMA tangu walipofukuzwa tarehe 28 November 2020 Baadae Baraza kuu kubariki maamuzi hayo tarehe 11 May 2022 baada ya rufaa yao kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati kuu ya CHADEMA kutupiliwa mbali na Baraza kuu la CHADEMA.
HAIWEZEKANI KUWA RAHISI
Mchakato baada ya hapo kwa mujibu wa katiba yetu, inasema vizuri kwa uwazi kabisa kuwa,endapo wabunge hao 19 watataka kurejea tena chamani baada ya Kuomba msamaha nini kitafanyika
Katika katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la 2019, Kanuni za Chama kifungu cha 6.5.4 ina sema
"Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza Kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu ya kutaka kurejea
Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata.
Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza kuu.
Watakaofukuzwa na Mkutano mkuu hawatokuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uwamuzi huo..".
Tafsiri yake ni kuwa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama; wabunge 19 wanatakiwa kurudi kwenye Kamati Kuu mmmoja mmoja au kwa pamoja kwa kuandika barua/maandishi kuomba kurejea kwenye Chama
Baadae Baraza Kuu kufanya uamuzi wa mwisho juu ya maombi hayo. Wala siyo kwa utashi wa kiongozi mmoja kama Mbowe,Lissu au Mnyika
HAIWEZEKANI KUWA SIRI
Baada ya mchakato huo mgumu wa Kikatiba ,Kamati Kuu inapaswa Kuitisha Baraza kuu au Kupeleka ajenda hiyo mbale ya Baraza kuu lenye wajumbe 423
Katiba ya CHADEMA ibara ya 7.7.11 inataja wajumbe hao 423 wote kwa nafsi zo ndani ya chama (a)Wajumbe wote wa Kamati Kuu (b) Makamu Mwenyekiti wa Kanda (c) Makatibu wa Kanda (d)Watunza Hazina wa Kanda (e) Wenyeviti wa Mikoa (f) Makatibu wa mikoa (g)Wajumbe Sita wa kuteuliwa na Mwenyekiti Taifa (h) Wajumbe watano wanaochagukiwa na Mkutano Mkuu wa Kila Baraza (i) Wenyeviti wa Wilaya (j) Makatibu wa wilaya.
Hawa ndiyo wanaofanya maamuzi ya Baraza kuu,ambapo kama kweli swala la Wabunge 19 lipo,maana yake wao ndiyo wangekaa kuwasamehe au kuwarejesha chamani
Lakini cha ajabu Wajumbe wa Kamati Kuu wanashangaa,Wajumbe wa Baraza kuu wanashangaa na wao wanatuuliza sisi wanachama kama ni kweli Wabunge 19 wamerejea CHADEMA
Wamesahau maamuzi ya mwisho kuhusu kuwafukuza wale wabunge 19 walifanya wao na kama siku wanatakiwa kurejeshwa maamuzi watafanya wao tena au kama kuwakatalia maombi ya kuwarejesha basi maamuzi hayo watafanya wao.
HALI HALISI YA WABUNGE 19
Kwa sasa wabunge 19 hawana mtizamo na msimamo wa pamoja juu ya hatima zao kisiasa wamegawanyika wala hawapo tena pamoja kama mwanzo
1.Kundi la kwanza limeshafanya maamuzi ya kuelekea CCM,Kwa maneno yao hadharani, kwa kuvaa sare za CCM na kushiriki vikao na mikutano ya CCM
Hapa wapo Nusrat Hanje,Jessa Kishoa,Esther Matiko,Hawa Bananga na wengine Sidhani kama hawa wanafikiri au wameshawahi Kuwaza kurejea CHADEMA
2.Kundi la Pili ni Wabunge ambao waliteuliwa kuwa ktk orodha ya Wabunge 19 lakini siyo maarufu wala hawana majina makubwa ya kisiasa
Hawa wameenda kuvuna pesa za bure na wanajua baada ya hapo siasa haiwadai,wala wao hawaidai
3.Kundi la Mwisho ni wachache wasiozidi wanne wanaotamani kurejea CHADEMA,wana ukaribu na mawasiliano na baadhi wanachama wa CHADEMA
Wanafuatilia kila kitu kinachohusu CHADEMA
Lakini wamekuwa wazito kufuata taratibu za hizo za CHADEMA
kwa mfano,sharti la CHADEMA la kuwataka Kujivua Ubunge huo haramu, kisha kuomba msamaha Baraza Kuu kama katiba inavyotaka.
Ili Baraza kuu liamue maombi yao juu ya kukataliwa au Kukubaliwa au kupewa masharti,mfano ya kuwarejesha CHADEMA kama Wanachama tu bila kupewa nafasi za uongozi tena kwa kipindi fulani kwa kadiri wajumbe watakavyo inafaa au kuamua kikaoni.
Je kwa kichwa cha Habari cha gazeti la Mwananchi kusema safari ya kina Mdee na wenzie kurejea nyumbani ipo kweli ...?
kama mpaka sasa hawajaandika barua au maandishi juu ya kuomba msamaha na kurejea CHADEMA..?
Boniface Jacob Ex-Mayor Mjumbe wa Kamati Kuu mstaafu. 0712 239 595
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA