Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kama NBC Premier League, inajiandaa kurejea kwa kishindo mnamo tarehe 16 Agosti 2024. Msimu huu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa wa kipekee, ukiwa na timu 16 zitakazopambana vikali kuwania taji la ubingwa. Maboresho makubwa katika vikosi vya timu mbalimbali yamefanyika, na kila timu inaonesha dhamira ya kuitoa Yanga SC kwenye kiti cha ubingwa.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kupitia Mtendaji Mkuu wake Almas Kasongo, imethibitisha kuwa ratiba kamili ya msimu itatangazwa ndani ya siku chache zijazo. Hata hivyo, tayari tunajua kuwa msimu utaanza rasmi tarehe 16 Agosti 2024, huku mechi ya Ngao ya Jamii ikipamba ufunguzi wa msimu kati ya tarehe 8 na 11 Agosti 2024. Msimu huu utakuwa na jumla ya mizunguko 30, ambapo kila timu itacheza mara mbili dhidi ya kila mpinzani, nyumbani na ugenini. Kilele cha msimu kinatarajiwa kufikia tarehe 24 Mei 2025.
Ratiba ya Mizunguko Ligi Kuu Tanzania Bara
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA