Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Kuna Taarifa kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, inakutana leo Jumamosi kujadili mashauri yaliyowasilishwa kwenye kamati hiyo ikiwamo sakata la Yusuph Kagoma na Awesu.
.
Kagoma anatajwa kusajiliwa Simba, huku Yanga ikipeleka pingamizi hawajarudishiwa pesa zao walizoilipa Singida FG (sasa Fountaine Gate) ili kunasa saini ya kiungo huyo.
.
Chanzo cha kuaminika kutoka kwa rafiki wa karibu wa Kagoma kimeiambia Arena, Yanga walilipa fedha za kumnasa Kagoma kwa klabu husika, lakini ilishindwana na mchezaji aliyekuwa amekubaliana na Simba kuingia mkataba wa miaka miwili.
.
“Yanga ndio wamepeleka pingamizi la kushinikiza Kagoma ni mchezaji wao kutokana na kutoa fedha kwa timu iliyokuwa inammiliki na mara baada ya kumalizana na Simba imeshindwa kurejesha kiasi cha fedha walichochukua kutoka Jangwani,” kilisema chanzo hicho.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA