Winga wa Yanga kutoka Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’, amesema amegundua mbinu mpya ya kupata muda zaidi wa kucheza kikosini.
“Kwa ushindani uliopo nimegundua kuwa ili niweze kuwa na nafasi zaidi lazima nifanye kitu cha tofauti kila ninapopata nafasi. Kila kocha atakaponipa nafasi lazima nionyeshe kuwa nilistahili kwa kufanya jambo ili kuweza kumfanya mwalimu anipe namba zaidi,” amesema Skudu.
Msimu uliopita akiwa Yanga Skudu hakuwa na nafasi ya kucheza kwa muda mrefu, kutokana na ushindani uliokuwepo, na sasa Yanga imesajili hivyo ushindani umeongezeka.
Hivyo huenda msimu 2024/25 ukawa mgumu zaidi kwa Skudu pale Jangwani, kama asipobadilisha aina yake ya uchezaji.
Yanga ya Gamondi haitaki mambo mengi, inataka wachezaji wasikae sana na mpira au kufanya udambwi usiokuwa na msaada kwa timu, haswa Skudu uchezaji wake ni huo wa kufurahisha majukwaa.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA